Monday, 30 April 2012

LADIES SATURDAY NIGHT OUT.......NYUMBANI KWETU CREW

mother house
violet na joyce wowowo
 
violet na maza house striking a pose
phillipina,violet na maza house
phillipina na violet
                       Nyikura toto la.......
grace na maza house tulikua tunasubiri msosi @ African village in birmingham
hilo ndo limsosi tulilokua tunalisubiri  maza house ndo wa kwanza kulidonyoa hahahhahahah
                                          ladies
  tulishibaaaa jamani siku ile kama upo diet tupa kulee ila nyama zao zilikua na pilipili bana arrrrg kama mtu utavisit hiyo african village waambie hao wapopo  unataka bbq meat without pepper other wise unapenda pilipili au mlevii
 after msosi we got ready tukajimuvuzisha kwenye club ya mablacks
  hapa watu wanacheza oliver twist wa d'banj
               watu walikua busy wanayarudi walikua bwaxxxxx

The Visit of Eto'o in People's Friendship University of Russia

Jumapili  tarehe 29.05 Mcheza mpira maarufu Samuel Eto'o alitembele jumuiya ya wanafunzi wa kiafrika wanaosoma chuo cha Urafiki Urusi. Eto'o alikua ni mgeni rasmi katika fainali za mpira wa miguu kwa nchi za kiafrika chuoni hapo.
Alipokua anaingia..(ulinzi ulikua mkali kiasi kwamba ikawa vigumu kupata picha)
Hapa akisalimiana na wasichana waliochaguliwa maalumu kumpokea "kitenge was the dress code"..Stephhh i see u baby  
Timu zilizoingia fainali Guinea (wenye nyeusi) na Guinea Ecuatorial (wenye nyekundu). Ambapo Guinea iliibuka kidedea kwa penalty
Hapa wanafunzi kutoka cameroon  wakiimba nyimbo za kwao, ikabidi na yeye anyanyuke akumbuke nyumbani kidogo. Eto'o aliejifunga sweta  shingoniEto'o akiingia kwenye gari kuondoka
Eto'o kwa sasa anachezea timu ya Anzhi Moscow Russia,ambapo analipwa 990m Tzshs kwa wiki.Na ni mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kuliko wote duniani.   

Sunday, 29 April 2012

DIAMOND ALIVYOTUA NA HELIKOPTA KWENYE UWANJA WA DAR LIVE......HAKUNAGA

Huyu ndie mwanamuziki anayebamba zaidi kwa sasa...


             Armando Christian PĂ©rez aka Pibull alipokua mdogo
                                                            Alivyo sasa
Huyu jamaa anapenda sana kuvaa suti. Video zake karibia zote utaona amevaa suti, na amenyoa kipara. Origin yake ni Cuba, na amezaliwa tarehe 15 january 1981.
                                                  Back in Time- Pitbull
Hii ni video mpya ya wimbo wa  Back In Time ambao  ni soundtrack ya movie mpya ya Men in black no3 inayotarajiwa kuanza kuonyeshwa tarehe 25 May. Kwenye hii movie tarajia kuwaona Will Smith, Lady gaga, Justin Bieber, Nicole Scherzinger na wengine wengi.

KILL ME PLEASE:PART ONE

TUNAENDELEA NA STORY YA KILL ME PLZ PALE ILIPOISHIA LAST SUNDAY
Hapo mwalimu likajitafutia mbinu ya kuwa karibu na Olga, likamuomba Olga apeleke vitabu vyake nyumbani kwake, binti wa wawatu bila kufikiria wala nn akakubali kwa heshima kubwa , alipofika nyumbani kwa mwalimu tu akalikuta hilo limwalimu limeshatangulia nyumbani ile olga kuingia ndani tu limwalimu likambaka msichana wa wa wa watu na kisha kumpiga mkwara kuwa akisema tu atamuua tena kwa mkono wake mwenyewe , mkwara huo ulimfanya Olga anyamaze na wala hakuwahi kumwambia mtu.....Bahati mbaya Olga kitendo cha kubakwa mara moja tu kwa vile hakuwa anajua mema wala mabaya akapata mimba..... na kama mnavyojua mimba hazijifichi mara moja akagunduliwa na kufukuzwa shule.... olga akarudi kwa mamaye akiwa mwenye masikitiko makubwa taabu na maisha ya pale kwao ni kitu kingine alichokuwa kikimuumiza sana but angefanya nini akajianzishia biashara yake ya kuuza mkaa somehow ndoto zake za kusoma zikazima kama vile nuru ya mshumaa inavyozima pale inapopulizwa na upepo......

Siku zilizidi kwenda hatimaye Olga alijifungua mtoto mzuri wa kiume aliyempa jina la Blessing..., japokuwa maisha yao yalikuwa ya shida but ujio wa mtoto somehow ulileta furaha fulani ndani ya nyumba , so wakarudi na kuwa watatu tena kama zamani, mtoto blessing aliendelea kukua vzr na akiwa mwenye afya njema, olga aliendelea na biashara ya kuuza mkaa na mamake akiuza mboga kwa kusaidiana waliweza kuishi maisha ya kawaida kabisa but still ya hali ya chini Baada ya miaka miwili mamake Olga alianza kuugua ugonjwa wa ajabu kila siku alikuwa akilalamika kuwa anaumwa na kichwa ,olga alimpeleka mamake hospital ili apate matibabu lkn mama alipata nafuu kidogo tu ila hakupona kabisa, akawa anaendelea kuumwa hivyohivyo tu , olga aliingiwa na uoga na akaapa kuwa hawezi kuacha mamake auugue hivyo coz hayuko tayari kumpoteza mamake no way mamake alihangaika naye sana so aliwaza kitu......

lazima nitafute kazi nitafute pesa ili niweze kumsaidia mama yangu, kwa bahati nzuri hapo kijijini kwao palikuwa na old friend ya mama yake alikuja kusalimia baada ya kuhamia jijini Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara na alipokuja salimia alisema ana rafiki yake tajiri mkubwa huko Mbeya anatafuta housegirl so kama kuna mtu yeyote angehitaji basi yy anaweza kwenda naye....Olga akajionea nafasi ndo hii wacha niende mjini nikatafute maisha so akamuaga mamake kwa masikitiko makubwa na kumwambia ucjali mom naenda kutafuta kazi ili nikusaidie uende hospital naomba wewe ukae na mwanangu mama naahidi mshahara wa kwanza tu nitawatumia wote ili muweze kupata mahitaji madogo madogo pamoja na pesa yako ya kwenda hospital

Kesho yake asubuhi na mapema Olga na yule mama wakaanza safari ya kwenda huko makao mapya, njiani alijiuliza maswali mengi ambayo hakuwa na majibu yake alijifikilia kwann anapata taabu zote anazozipitia ni wapi alikomkosea mungu hadi awaadhibu kwa taabu zote hizo na je ni nini hatima ya maisha yao, alianza kujifeel kuwa anamiss sana nyumbani ndani ya siku ile moja tu alimmis sana mwanae na akawa akimfikiria sana mamake ambaye alimuacha akiwa anaumwa huko nyumbani , anyway somehow alijikuta akijipa moyo kuwa huenda hivyo ni vipimo tu katika maisha na may b one day maisha yao yatabadilika na kuwa sawa na ya watu wengine Walifika Mbeya usiku wa maneno na wala hata hakuuona mji vizuri na moja kwa moja alipelekwa huko kwa boss mpya ambaye alikuta wamelala so alifunguliwa geti na walinzi naye akaonyeshwa sehemu ambayo alijitupia hivyo hivyo na tunguo twake tuchafu na kulala akiwa mchovu sana, then asubuhi alishtuliwa na maji ya bariiidi ambayo alimwagiwa na boss wake mwanamke na kuulizwa wewe hapa umekuja kufanya kazi au kulala! Alikurupuka na kujibu kwa sauti ya upole shikamooo mama, matherboss baada ya kujibu alisonya na kumrushia nguo na kumwambia hebu niondokee kaoge huko usije kuwaambukiza wanangu chawa!

 Olga alichukua hizo nguo na wala hakusema kitu akaenda kuoga na kubadirisha nguo kisha akaonyeshwa linyumba lote na makazi yote jinsi ya kufanya then akaingia kazini siku hiyohiyo , alifanyishwa makazi weee nusu aanguke klwa kizunguzungu lkn kila alipokuwa akikumbuka shida za nyumbani kwao wala hakujali alifanya kila kitu kwa moyo mmoja kabisaa alikaa kama siku tatu hv bila kumuona baba wa nyumba kumbe alikuwa amesafiri kwenda kusalimia wazazi wake alisafiri pamoja na wanae wawili wa kiume so siku ya nne baba mwenye nyumba alirudi na alipokuja alimchangamkia Olga vzr tu akamsalimu na bahati watoto wake nao walitokea kumpenda sana olga na walimuita dada so some how familia ikawa imepata mdada mzuri sana japo mama mwenye nyumba tu ndo alikuwa taabu.......... JE MAMA MWENYE NYUMBA NA OLGA HATIMA YAO NINI??? USIKOSE KUFATILIA STORY HII NEXT SUNDAY............ TO BE CONTINUED


MTUNZI-NYEMO DAVID.

Saturday, 28 April 2012

WANASEMA IF YOU GOT IT, FLAUNT IT: NICKY SHOWS OFF HER HOURGLASS FIGURE IN STARSHIPS VIDEO



uongo mbaya huyu dada kajichonga vizuri aisee i know its not her really figure but she got it ma'aam its better of the surgery figure kuliko kuwa na yamchina maana ipo siku itachina lol,
That's how nicky dressed kwenye shooting ya video mpya ya starships iliyofanywa huko hawaiii she really rocks babyy!!

Wednesday, 25 April 2012

Nani mkali hapa Wema Sepetu au Rihanna!!??


Hapa tunalinganisha Nywele tu,wote wamekata nywele pembeni kidogo....nani hii style imemtoa zaidi??Wema au RiRi??? 

Haya jibu la high heels limepatikana


Madaktari wamegundua tiba inayoweza kumfanya mwanamke aweze kuvaa viatu vyenye mchuchumio "high heels" bila kusikia maumivu.Huduma hiyo 'Toe job" inagharimu £320 ambayo ni sawa na laki 7.3 tsh. Toe job inachukua muda wa dakika 20 kukamilika, na hudumu kwa muda wa miezi sita.
Hapo sasa, Boob job, Lip job, Butt job na sasa Toe Job imeingia...kazi ipo.

Monday, 23 April 2012

Happy Anniversary Marwa and Hubby

What a lovely couple!!!....Congratulations,Mungu awajalie amani na upendo kwenye familia yenu. Inshallah

Sunday, 22 April 2012

KILL ME PLEASE: PART ONE

KATIKA MAISHA KUNA WATU WANAVIPAJI LAKINI HAWAJUI WAPI PAKUANZIA ILI WATOKE  KATIKA PEPESA PEPESA MACHO YANGU KWENYE MAKUNDI FULANI FULANI KATIKA FACEBOOK NILIKUTANA NA WADADA WENYE UWEZO WA KUWEZA KUTUNGA STORY ZAO WENYEWE  NA ZINASISIMUA HASWAA. BLOG YA NYUMBANI KWETU ITAKUA INAKULETEA STORY MBALI BALI KILA SIKU YA JUMAPILI KAMA UNAPENDA STORY KAMA ZA KINA SHIGONGO BASI HAPA UTAPATA UHONDO WA AINA YAKE LEO TUTAANZA NA STORY INAITWA KILL ME PLEASE NA MTUNZI NI NYEMO DAVID YEYE ANAUWEZO WA KUTUNGA FILAMU KALI KALI KUHUSIANA NA JAMII INAYOTUZUNGUKA HAYA PATA MAUTAMU.COM ( spare the grammatical errors)

KILL ME PLEASE: PART ONE

Nakushangaa unavyotaka kumuua huyo mtoto, ni mdogo sana na hana hatia kama unavyofikilia , kwa nini usiniue mimi badala yake! but plz usisahau sometime unaweza kumuua mtu anayekupenda kuliko unavyofikiria wewe, and i want to conferse to u that i love u! and am very happy to die while am in love with u....Olga aliyasema maneno hayo huku sura yake ikiwa imejawa na woga uliochanganyika na mapenzi ya dhati kwa jambazi hilo , je kwann Olga alilazimika kusema hayo plz fuatilia story hii inayokujia kwa hisan kubwa ya NYEmo Daaaavid.......
Olga, olga, olgaaaaaaaaaaaaaaaaaa eeeeeeeeeeeeeh hebu njoo bwana yaani husikiii ninavyokuita hivi wewe mtoto mbona unaniletea ujeuri siku hizi? Mama Olga anamuita bintiye mbaye kwa muda huo yuko chumbani anajifanyia home work zake , olga ni msichana wa miaka 16 na ametoka katika familia ya kimasikini mama samahani nilikuwa namalizia homework zangu, vp unasemaje mom,?mama samahani nilikuwa namalizia homework zangu, vp unasemaje mom,? Ok Olga naomba kesho uchelewe kdg kwenda shule ukae na mdogo wako miye nataka niende kwenye biashara zangu, mama ake Olga alikuwa anajishughulisha na uuzaji wa mboga ya kisamvu alichokuwa akienda kukichuma katika mashamba ya watu , Mama Olga alizoea kila siku asubuhi na mapema kumbeba mwanae ambaye alikuwa na mwaka mmoja na nusu kisha kwenda kwa marafiki zake waliokuwa na mashamba jirani, mama Olga aliwasaidia kidogo kazi , kisha nao kama kumpa asante walimruhusu kuchuma kisamvu ambacho alikuwa akienda kukitembeza katika manyumba ya watu na pesa alizozipata zilimsaidia katika kujikwamua na maisha magumu yaliyokuwa yakiwakabili hapo nyumbani......

Baba yake Olga alishawakimbia siku nyingi baada ya kuona maisha yamekuwa magumu pale nyumbani akaenda mkoa mwingine kuanza maisha mapya huko, kwa hiyo aliwaachia familia yake maisha yasiyokuwa hata na matumaini, lkn pamoja na hayo yote olga hakukata tamaa kwenye kujituma ! alisoma kwa bidii zote shida za pale nyumbani hazikumfanya alegeze uzi alijitahidi sana kwa kuona kuwa may be kwa kusoma kwake Mungu angekuja kuyageuza maisha yao hapoo baadae..... Olga alipoingia darasa la saba maisha yalizidi kuwazidia , na kuwa magumu at the same time Olga alitakiwa awe na vifaa vya shuleni kitu ambacho kilimuongezea mama yake gharama ,Olga alionekana kumuonea huruma sana mamake but hata hivyo angefanyaje? ihali yeye bado ni teneeger hakuwa hata na idea maisha ya nje yanaendaje kitu alichokiamini yeye ni shule na ndo maana alionyesha bidii zake zote! Olga alifanikiwa kufanya mtihani wa darasa la saba ambapo baadae majibu yalikuja na kuonyesha kuwa alikuwa miongoni mwa wasichana wachache hapo shuleni kwao waliochaguliwa kujiunga na elimu ya secondari, habari hizo zilileta mchanganyiko wa furaha na huzuni kwani hawakuelewa wangepata wapi pesa za kununua vifaa vya shule Wakiwa ktk kutafakari, mama Mayasa ambaye alikuwa ni best friend wa mama ya Olga alikuja na Idea kuwa kwann mama Olga asijaribu kupika pombe za kienyeji na kuwauuzia watu! maana hizo atleast angeweza kupata kipato cha kumnunulia bintiye vfaa vya shule, Idea hiyo ilipokelewa vzr na mama Olga kwa msaada mkubwa wa rafikiye mama Mayasa walianza kujiandaa kwa ajili ya kupika pombe hiyo kwanza walikoka moto mkali wa makuni , kisha wakatumbukiza maji ktk pipa kubwa na unga wakaanza kuyachemsha, huo mchanganyiko ulichemka kwa siku nzima, then jioni kama saa kumi na mbili wakayaipua mamchanganyiko hayo ili kuyapooza ndo wachanganyie na mchanganyiko mwingine hadi next day inakuwa pombe tayari, sasa walisaidiana na kuyaipua then wakagawanyisha katika mapipa mengine mawili ili upoe na then wakawa wanajaribu kupooza mara kwa mara , sasa ktk kupooza mdogo wa Olga alikuwa akipita pita katika kucheza na kwa bahati mbaya wazazi wake walijisahau na kufanya mambo mengine kwa bahati mbaya mtoto alikorofisha pipa moja na ule mchanganyiko wote ulimwagika na kumwagikia mtoto! tahamaki mama olga alijitahidi kumbeba mwanae na kumkimbiza hospital lkn kwa bahati mbaya madaktari walishindwa kuokoa maisha ya mtoto kwani alikuwa amebabuka mwili mzima kwa hiyo mtoto alipoteza maisha!Msiba wa mdogo wa Olga uliwaumiza sana watu, asubuhi na mapema kila mtu alikuwa akielekea kwenye msiba mama ya Olga alilia sana kwa kumkosa mwanae Olga naye alilia sana na alijilaumu kwa yote hayo yalitokea kwa sababu yake alimuhurumia sana mama yake kwa kupoteza mtoto ilimradi tu amsaidie olga aende shule, watu walikuja na kutoa pole nyingi kwa wafiwa , mama alizihifadhi hipo pole zote na baada ya msiba kwisha alizitumia pesa hizo ili kununua vfaa vya mwanae na hivyo ndivyo Olga alipoanza kidato cha kwanza kwa masikitiko makubwa moyoni alifikiria yaani mdogo wangu amejitoa sadaka ili tu nifanikiwe hakika nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu ili nije kuyaenzi maisha ya mdogo wangu

Olga alifanikiwa kwenda shule na kuanza kidato cha kwanza huku akiwa na matarajio ya kujiendeleza ,na alijitahidi sana katika masomo yake hadi akaanza kuwashangaza walimu wake na mamake aliendelea na biashara yake ya kuuza mboga biashara ya pombe hakuitamani tena kwani ilimsababishia akampoteza mtoto wake aliyempenda sana , but biashara yake haikuwa nzuri tena kwani pesa alizokuwa anazipata ni kwa ajili ya kula tu so maisha yalianza kumuelemea sana hata hivyo jambo la kumshukuru mungu alikuwa peke yake tu kwani binti yake alikuwa ameenda shule so tumbo la mtu mmoja halikumpa shida sana Bahati mbaya ilianza tena olga alianza kukosa vifaa vya shule na kama mnavyojua hakuna hata mtu wa kumpiga jeki na hali hiiyo ikaanza kumfanya akate tamaa ya maisha, mwalimu Kipepe ambaye alikuwa ni mwalimu wake wa jiografia aliiugundua hali hiyo mara moja akaanza kutafuta mbinu za kumpata binti wa wawatu , kwanza alianza kwa kumpatia vijizawadi vya hapa na pale Olga hakuwa na wasiwasi kwani aliamini mwl alikuwa akimsaidia kwa nia njema kabisa na one day mwalim alimwambia olga kuwa Binti usiwe na wasiwasi nimeshapokea ada yako mama yako alishanitumia so we endelea vzr na shule wala usiwaze habari ya ada kumbe alikuwa anamdanganya hakuna ada iliyotolewa wala nini
TO BE CONTINUE..........

 
 
 
.
 

Saturday, 21 April 2012

this is to all those who are heartbroken...

Better In Time -Leona Lewis
There is a day you will forget everything, and life will go on.Time heals the pain.enjoy ya weekend people. 


lady jaydee ft mr blue-wangu

Rihanna vipi tenaa!!???

Jana Rihanna alitweet "'first date in two years"  Ok, was happy kuona kua RiRi went back on her feet na kuamua kudate baada ya story nyingi kumuhusu, ikiwemo ya kurudiana na Chris Brown kisirisiri.Na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa jana

Rihanna na best friend wake Melissa Forde jana wakitoka kwenye date yao iliyofanyika jana. na  baada ya hapo RiRi alimtweet Melissa "datenight my lover for the night @mforde11 
Rihanna amekua akitwaja kuwa Lesbian na kua na mahusiano ya kimapenzi na rafiki yake huyo wa kike  mara kwa mara. Na tuhuma hizo zilizidi baada ya kutoa wimbo wa Te Amo ambao unazungumzia mahusiano ya kimapenzi baina ya wanawake wawili. 

Thursday, 19 April 2012

NI MARUFUKU KUMTEMBELEA LULU MAHABUSU, UWAZI KUHUSU KESI YA KAJALA


JESHI la Magereza nchini limepiga marufuku watu wasiokuwa na uhusiano na msanii chipukizi wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kumtembelea katika mahabusu ya Segerea.
Lulu anashikiliwa katika gereza hilo kwa tuhuma za mauaji ya msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba baada ya kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.
Habari zilizotangazwa na kituo cha Radio One jana zilieleza kuwa, kwenye ubao wa matangazo ndani ya gereza hilo, kumeandikwa barua inayotoa maelekezo kuhusu watu wanaopaswa kumuona Lulu.Kwa mujibu wa barua hiyo, watu wanaopaswa msanii maarufu wa filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe Faraji Chambo inatarajiwa kuwa na mashahidi 13 na vielelezo tisa.Kajala na Chambokumtembelea Lulu kwenye mahabusu hiyo ni mama yake mzazi, dada yake na mjomba wake, ambao picha zao zimebandikwa kwenye ubao huo wa matangazo.“Watu wamezusha sana maneno kuwa, askari wamepiga marufuku hakuna mtu yeyote kumtembelea Lulu, ni uzushi tu,” alisema mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho aliyetembelea kwenye mahabusu hiyo juzi.Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha Kanumba, aliyefariki usiku wa kuamkia Aprili 7 na mazishi yake kufanyika Aprili 10 mwaka huu. Alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa mara ya kwanza wiki iliyopita na kesi yake itatajwa tena Aprili 23 mwaka huu.Wakati huo huo, upande wa mashitaka katika kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili  walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo.
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Leonard Swai alidai kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao.
Katika maelezo hayo, washitakiwa walikubali baadhi ya mambo kuwa ni mume na mke, waliuza nyumba kwa Emiliana Regarulila na Chambo alikubali alikuwa ni mtumishi wa benki ya NBC mwaka 2008.
Washitakiwa walikataa kupewa notisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wasiuze nyumba hiyo kwa sababu ilikuwa kwenye uchunguzi, hawakwenda kinyume na notisi hiyo na kumuuzia nyumba Emiliana.Mambo mengine waliyokataa ni kwamba hawakuhamisha nyumba hiyo kwa Emiliana kwa kutumia fedha za rushwa.
Swai alidai wanatarajia kuwa na mashahidi hao na vielelezo hivyo na Hakimu Mkazi Sundi alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Aprili 30, mwaka huu
             HABARI FROM: AMANI MASUE BLOG

pic of the day: baby Aleesah

keki yakwatwa sehemu nyeti kurepresent a black woman circumsion HOW SAD!!!!!!




                                                                     
            
this is one of the news that has really shocked nakunifanya nijisikie vibaya mm kama msichana wa kiafrika. huyo mama kushoto anaitwa   Lena  Adelsohn Liljeroth  ni minister of culture huko sweden ameonekana akikata sehemu nyeti za keki iliyodizainiwa na Makode Aj Linde which  the cake was about an african women circumsion kitendo cha kukata keki hiyo sehemu nyeti imeonekana kama  ni kitendo cha uracist maana lena alionekana kufurahia, making jokes na kula keki bila kujali chochote though walipomuuliza alisema yeye asilaumiwe as alifanya alichoambiwa na disigner wa keki hiyo. THIS IS TOTALLY RACISM N FOREVER RACISM WILL NEVER STOP AS WAZUNGU STILL THINK THEY ARE MORE SUPERIOR THAN BLACKS 
ingia humu ujionee   http://bcove.me/qqgbpfcok                             

Wednesday, 18 April 2012

couple of the day...


Jennifer, huby wake David senior and baby wao David Jr
 Jennifer Hudson na mtoto wake David Daniel Otunga Jr...isn't the baby cute!!?? and He got swags (mama Jamal upo?)

Tuesday, 17 April 2012

Happy Birthday my beautiful girls

                                                                           Judith
                                                                      Anitha
                                                                             Prisca
                                Enjoy your day girlsss...

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet