Saturday, 28 January 2012

nipo njia panda naombeni ushauri please!!!!!!!!!!!

halo wadau,
mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 nilikua na mpenzi wangu kwa takribani miaka 6 na tulifanikiwa kupata mtoto mmoja katika mahusiano yetu lakini hatujaoana, familia ya mume wangu haikunipenda kabisa kutoka na familia zetu kuwa tofauti katika masuala ya uchumi.mpenzi wangu alitokea kuishi katika familia yenye uwezo sana na mm nimetokea katika hali ya kawaida yani medium class mama mkwe wangu kahunipenda kabisa ila mwanae alinipenda sana.bahati mbaya au nzuri mpenzi wangu alipata safari ya kwenda uingereza kujiendeleza na masomo yake ya masters   tulikuwa tukiwasiliana vizuri tu ila baadae mpenzi wangu alikata mawasiliano ghafla na alikua akirudi tz alikua hanitafuti kabisa. nilikata tamaa na kuanzisha mahusiano na mwanaume mwingine. yupo tayari kulea mwanangu na nina furaha na maisha yangu tatizo huyo bf wangu wa  mwanzo karudi kimoja na anasema anataka kunioa nilipomuuliza kwa nn alikua ananifanyia yote hayo eti ni kwa sababu alikua ananipima penzi langu kwake je nikubali kurudiana nae au niachane nae naombeni ushauri please nisije nikamuacha huyu halafu nikaachwa kwenye mataa
email yangu kapuni please!!!!!!!!!!!!!!

4 comments:

  1. usitape tape tuliza akili na ujue nani anakupenda huyo aliekutelekeza mchunguze sana

    ReplyDelete
  2. usidanganyike na huyo wa ulaya...alikua wapi siku zote?mtu akupendae hawezi kukupima kwa style hiyo. usitupe bigijii kwa karanga za kutafuna...

    ReplyDelete
  3. kwa ushauri wangu mi ni bora uendelee na huyu mopya ambae ameshaweka na nia ya kukuoa,coz sidhani kama huyo ana mapenzi ya dhati tena na wewe,huenda ikawa anafanya hvyo tu kwa kuona lbd nafasi yake ya ubaba inachkuliwa na mwengine,SIDHANI KAMA NI JAMBO LA BUSARA KURUDI KWA HUYO WA MWANZO!

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu achana na huyo wa London, kama alishakutenda nia yake ni wewe upate tabu na ukose raha, amekuona unafuraha ndo anataka akuharibie, na kama mama mkwe hakua akikupenda ndo kabisaaaa, achana na huyo mwanaume na mkubali huyo aliyeonyesha pendo la dhati na kuwa tayari kulea mtoto wako

    ReplyDelete

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet