Wednesday 15 February 2012

Mapishi ya Sponge Cake

Mahitaji

Mayai 4( Tenganisha kiini na ute)
kikombe 1 cha sukari nyeupe
Vijiko vya chakula 4 vya maji baridi
Kikombe 1 chya unga wa ngano uliochekechwa.
Kijiko kidogo 1 cha baking powder
Kijiko 1 kidogo cha vanila au ganda la limao

Jinsi Ya Kuandaa
1..Washa oven kwa joto la centigrade 175.
2.Weka viini vya mayai ktk bakuli kubwa na uchanganye na sukari na vanila au ganda la limao lililokwanguliwa (hii kwangua kule kwa kijani au njano tu) usikwangue weupe) Koroga mpaka mchanganyiko uanze kubadilika rangi na kuwa kama mweupe.
3.Ongezamaji na ukoroge mpaka vichanganyike.
4. chukua chombo chenye ute wa yai na ukoroge mpaka litokee povu jingi jeupe. Kisha miminia ktk mchanganyiko wako wa mwanzo na ukoroge tena mpaka vichanganyike.
5. Chukua chombo cha kuokea na ukipake siagi kisha unyunyuzie unga wa ngano. Mimina mchanganyiko wa cake ktk chombo cha kuokea na uoke kwa muda wa nusu saa mpaka dk 40.
 6. choma cake yakokatikati kwa kutumia kisu chenye ncha kali na kisu kikitoka bila kunata ujue cake yako imeiva, kikitoka kinanatanata ongeza muda kama dk 5-10 na uipue..


 maandalizi


Cake ikiwa tayari kwa kuliwa.
ANGALIZO
Kama unahitaji cake kubwa zaidi fanya hivyo vipimo mara mbili ,tatu au nne kutegemea na ukubwa uutakao
Asante Celine kwa recipe.

No comments:

Post a Comment

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet