Tuesday 14 May 2013

POLE FLORA BAHATI LYMO AKA MBUTA NANGA




BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya karne.
      Katika uchunguzi wake, hivi karibuni gazeti hili lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.

VYANZO
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.

MAZITO
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).

MAZOEA YAANZA
Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake  nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.

KISA KUJISAIDIA HAJA NDOGO
“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.

HADI KITANDANI
Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”

AITA POLISI
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”

UBAKAJI/KUTISHIA KUUA
Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.
“Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.
                         MORE STORY BOFYA HAPA
                           http://www.globalpublishers.info/
                         http://missfbknitwearlyimo.blogspot.co.uk/

 

 

No comments:

Post a Comment

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet