Msanii wa kike wa filamu
Tanzania Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu,amefikishwa mahakamani
akikabiliwa na mashtaka ya mauaji kikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwingine wa filamu Marehemu Steven
Kanumba.
Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne,
tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa
walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta
ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini
ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa
wamejihami kwa silaha
Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai
mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la
Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven
Kanumba.
Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo
kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu
mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji
anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu
wake.
Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa
miaka 18 baada ya kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17,
hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa
msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama
mshtakiwa.
Kesi hii ya mauaji inatajwa
kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko
kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka
huu.
Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku
hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.
Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa
mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi
wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio
lenyewe.Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa
shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba
kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa
kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata
nchi za nje.
source YOU BEEN SNAP BLOG
Kweli kifo hakikosi sababu, mm siamini kama Lulu anaweza kumuua Marehemu, ninacho amini ni kwamba siku zake zilifika. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, na Lulu aachiwe huru!
ReplyDelete