Jumapili tarehe 29.05 Mcheza mpira maarufu Samuel Eto'o alitembele jumuiya ya wanafunzi wa kiafrika wanaosoma chuo cha Urafiki Urusi. Eto'o alikua ni mgeni rasmi katika fainali za mpira wa miguu kwa nchi za kiafrika chuoni hapo.
Alipokua anaingia..(ulinzi ulikua mkali kiasi kwamba ikawa vigumu kupata picha)
Hapa akisalimiana na wasichana waliochaguliwa maalumu kumpokea "kitenge was the dress code"..Stephhh i see u baby
Timu zilizoingia fainali Guinea (wenye nyeusi) na Guinea Ecuatorial (wenye nyekundu). Ambapo Guinea iliibuka kidedea kwa penalty
Hapa wanafunzi kutoka cameroon wakiimba nyimbo za kwao, ikabidi na yeye anyanyuke akumbuke nyumbani kidogo. Eto'o aliejifunga sweta shingoniEto'o akiingia kwenye gari kuondoka
Eto'o kwa sasa anachezea timu ya Anzhi Moscow Russia,ambapo analipwa 990m Tzshs kwa wiki.Na ni mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kuliko wote duniani.
cool! but check out about the language
ReplyDelete"waliochagulia= waliochaguliwa?"
pia
Jumapili ya tarehe 29.05 mwezi wa tano haujafika au tarehe ya kichina hii..
uchune bwana sio kila kitu lazima utue kasoro eeeh
ReplyDelete