Sunday, 20 May 2012

MISS TANZANIA-UHONDO FROM LAST SUNDAY

tuko na Vero na Vick kwa hiyo wanatakiwa wasi hisi kitu chochote.Mimi nitakuwa macho
kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kitakachoharibika “
... “Usihofu Andrew nalifahamu hilo na niko makini nalo sana.naelewa leo ni siku ya kipekee maishani
mwangu.Ni siku ya kihistoria katika maisha yangu hivyo siwezi kuiharibu.”
Baada ya kumaliza kujiandaa na kuhakikisha kuwa wako safi wakaingia garini na kueleka Diamond
Jubilee.
**************************************************************
Ukumbiwa Diamond jubilee ulikuwa umefurika watu pasi mfano.Pamoja na ukumbi kufurika watu bado
watu walikuwa wakmiminika ukumbini hapo kwa lengo la kushuhudia mchuano wa kumtafuta mrembo wa
Taifa atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya dunia.
Patrick,Vero,Andrew na Vick waliwahi sana kuingia ukumbini na kuchukua moja kati ya meza za mbele
kabisa.Patrick moyo ulikuwa ukimdunda sana usiku huo,.Andrew alilifahamu hilo na hivyo akawa
makini sana katika kuakikisha kuwa hakuna kitu kitakachoharibika .Toka wameingia ukumbini Patrick
alikuwa kimya .
“Patrick are you ok?Vero liuliza baada ya kuona Patrick yuko kimya sana.
“Yes I’m ok Vero usihofu.”
Mara muongoza shughuli akatokea jukwaani na kuanza kutangaza.
“Mabibi na mabwana mliohudhuria mashindano haya makubwa ya urembo nchini napenda kuwakaribisha
sana katika usiku huu wa pekee kabisa kwetu sote.Ni usiku wa pekee kwa sababu leo tutaandika
historia mpya

historia mpya kabisa katika mashindano ya urembo hapa nchini na ulimwengu kwa ujumla.Kwa mwaka huu
kamati nzima ya Miss Tanzania imeazimia kufanya mabadiliko makubwa sana na nyie wote mlioko hapa
ndio mtakaokuwa mashahidi wa kile kitakachotokea usiku wa leo.Nasema karibuni sana katika usiku
huu na tujumuike sote mimi naitwa Mc Thora kwa wale ambao hawanifahamu..
“Mabibi na mabwana kabla hatujaendelea mbele na ratiba yetuningependa kwanza kumkaribisha
jukwaani mkurugenzi mkuu wa Sean woris entertainments ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano
haya kwa mwaka huu Mabibi a mabwana makofi kwaaaa Mr Petty.s Woris”
Petty woris mkurugenzi wa sean woris entertainments akapanda jukwaani akiwa amevalia nadhifu
kabisa.
“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,viongozi mbali mbali na wote mliohudhuria mashindano haya
usiku huu asalam aleikhum.Ni furaha ilioje kwetu sisi kama Sean woris entertainments ..




...kudhamini
mashindano makubwa kama haya ya urembo hapa nchini.Kama wote mnavyoshuhudia mashindano ya mwaka
huu yamekuwa na utofauti mkubwa na mengine yaliyotangulia.maandalizi yake yamekuwa mazuri ,zawadi
zimeboreshwa na ushindani miongoni mwa washiriki umeongezeka mara dufu.Kwa kuwa ni mara yetu ya
kwanza kudhamini mashindano makubwa kama haya bado kunaweza kuwa na kasoro kadhaaambazo nina
imani kwa kushirikiana na wadau wote wa urembo hapa nchini tutasaidiana kuzitatua.Nina imani bado
tutaendelea kudhamini na kuandaa matamasha mengi na makubwa zaidi hapa nchini ili kuzidi kuukuza
wigo wa burudani hususani sanaahii ya urembo.Mwisho kwa niaba ya uongozi na wafanya kazi wote wa
Sean woris entertainments napenda kuwatakia wote utazamaji mzuri wa mashindano haya usiku
huu.Ahsanteni sana.”
Baada ya kumaliza akarudisha kipaza sauti kwa muongoza shughuli kisha akashuka jukwaani.
“mabibina mabwana huyo alikuwani mkurugenzi wa Sean woris entertainment ambao ndio wadhamini
wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu..Mabibi na mabwana kwa mujibu wa ratiba yetu kinachofuta
kwa sasa ni kuwatambulisha majaji wa mchuano huu ambao ndio watakaofanya kazi kubwa na ngumu ya
kutuchagulia mrembo mwenye sifaya kuwa mrembo wa taifa.Majaji tulionao usiku huu ni
saba.Ningeomba jaji utakaposiia jina lako likitajwa basi usimame ili watu wakufahamu.Wa kwanza ni
Mr Ernest Namesha,wa pili ni ndugu Mecky ,tunaye pia Mr Boniventure Gregory,anayefuatia niMr
Samweli Nathaniel,tunaye pia dada yetu mpendwa usiku huu naye ni dada Esther mdee,pia tunaye Mrs
Coletha brown,tunaye vile vile bi Susan Abrahams na wa mwisho ni ndugu Jacob Lyimo.Hawa ndio
majaji wetu ambao watakuwa wakifanya kazi ngumu ya kumchagua mrembo wa Taifa usiku huu wa leo.”
“mabibi na mabwana baada ya kuwafahamu majaji wa mchuano hu wa leo sasa naomba niwalete kwenu
warembo wote 26 katika show maalum waliyoiandaa “
wimbo ukaanza kupigwa na warembo wakaanza kutoka huku wakicheza kwa stailiyenye kuvutia
sana.makofi nderemo na vifijo vikatawala ukumbini.Patrick alielekeza macho na akili yake yote
jukwaani na bila kukosea alimuonahappy ambaye alikuwa amependeza kupindukia Jasho
likaanzakumtiririka akatoa kitambaa na kujifuta.Alikuwa imya kabisa.
Baada ya show ya warembo kukamilika ziliendelea burudani mbili tatu toka kwa wasanii mbali mbali
kisha muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“Mabibi na mabwana baada ya kupata burudani hizo zakukata na shoka sasa naomba niwalete kwenu
warembo wote 26 ili muwatambue.Watapita hapa jukwaani mmoja mmoja .”
Warembo wakaanza kutoka nyumaya jukwaa na kuanza kupita mbele ya watazamaji.Kidogo Patrick atamke
kitu baada ya kusikia jina la Happy likitajwa .Happy akapita jukwaani huku kelele za shangwe
zikisikika.Happy alikuwa akionekana kama malaika usiku huu.alikuwa amependeza vilivyo.Kila mtu
aliustaajabia uzuri wa binti huyu mwenye kila sifa ya kuwa mrembo wa Taifa na dunia.Kelele zile za
mashabiki zilizidi kumchanganya Patrick na kumfanya ahisi kuchanganyikiwa.Andrew alikuwa makini
sana kwa lolote ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani kati yao.
Baada ya kupita jukwaani kujitambulisha kwa mashabiki zikafuata burudani za aina yake toka kwa
wanamuziki.Kisha Muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
“mabibi na mabwana mambo yanazidi kupamba moto.Mambo ni bam bam na kama ...

Mambo ni bam bam na kama nilivyowaeleza toka mwanzo
kuwa Sean woris entertainment wameleta mageuzi ...

...makubwa katika mashidano ya mwaka huu .Kwa sasa
napenda kuwaleta kwenu warembo wote 26 wakiwa katika vazi la ufukweni.Mhh hapa pana kazi kweli
kweli .mabibi na mabwana hebu tuwashangilie hawa warembo wetu watakapokuwa wakipita jukwaani
katika vazi la ufukweni.”
Warembo wakaanza kupita jukwaani wakiwa katika vazi la ufukweni.Siyo siri walikuwa wamependeza
vilivyo.Baada ya kumaliza kupita navazi la ufukweni zikafuata tena burudani halafu warembo wote
wakapita tena kwa mara nyingine na vazi la ubunifu.Kelele zilikuwa kubwa sana kila walipopita
warembo Neema wa Arusha na Happy wa Ilala.Warembo hawa walionekana kuchuana vilivyo.Kisha pita
na vazi la ubunifu muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“mabibi na mabwana tayari tumewashudia warembo wetu 26 wakipita hapa mbele yetu wakiwa katika
mavazi tofauti tofauti.Kwa sasa ule wakati mliokuwa mkiusubiri kwa hamu kubwa unaelekea
kuwadia.Kwa hivi sasa tutakwendakuwafahamu warembo 10 bora ambao wameonekana kufanya vizuri zaidi
.Naomba sasa nimkaribishe Mrs Coletha brown ili aje atutangazie wale warembo wetu kumi waliofanya
vizuri zaidi.Karibu sana mama.”
Mrs Coletha brown akapanda jukwaani akiwa na karatasi yenye majina ya warembo kumi waliofanya
vizuri na ambao wataendelea na mchuano.
“mabibi na mabwana napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuwapongea waandaaji wa mashindano haya
ambayo kwa mwaka huu yameboreshwa kwa kiwango cha juu kabisa.
Mabibi na mabwana kazi yetu usiku wa leo imekuwa ni ngumu sana .Warembo wote wako katika hali ya
ushindani wa hali ya juu mno.Lakini tumeweza kuwapata wale kumi ambao ni bora zaidi na ambao
nitaenda kuwataja hivi punde.Nambari 12 Nelea shulo,nambari 9Saida abdi,nambari4 Upendo
timelo,Nambari 20 Neema i,Nambari 11 Esther stevens,Nambari 6 Happy ,nambari 22 Elimeena
kimuo,nambari 26 bahati udhoka,nambari 16 Winifrida mwasajuki,na mwisho ni namba 13 genevieve
alphonse.”
Kelele za kushangilia zikasikika ukumbini.Warembo waliofika hatua ya kumi bora wakajipanga
mstari.wakapiga picha ya pamoja kisha zikafuata burudani .baada yaburudani mc akapanda tena
jukwaani.
“Mabibi na mabwana bado tunaendelea na mchakato wetu wakuifikia ili hatua kubwa kabisa ambayo
kila mmoja wetu aliyeko hapa anahamu ya kuishuhudia.Kila mmoja anatamani amfahamu mrembo wetu mpya
wa Taifa.Kwa sasa tutaenda kuwatafuta wale watano bora ambao kutoka kwao tutampata mrembo
wetu.Atapanda tena Mrs Coletha kuja kututangazia warembo watano bora .”
mrs Coletha akapanda tena jukwaani akiwa ameongozana na watu wawili wa miraba mine wanaomlinda.
“mabibi na mabwana kama nilivyowaambia kuwa kazi yetu leo imekuwa ngumu sana hasa kutokana na
jinsi warembo wote walivyo na vigezo vya juu mno kiushindani.Lakini pamoja na wotekuwa na
ushindani wa juu tumeweza kufanikiwa kuwachuja na kupata wale watano ambao wameonekana kuwa ni
bora zaidi.
Warembo waliopita hatua ya tano bora ni mrembo nambari 16 Winifrida mwasajuki,nambari 20 Neema
i,nambari 13 Genevieve alphonse,nambari 26 Bahati udhoka na mwisho ni nambari 6 Happy .”
Kelele kubwa zikasikika zikishangilia.Kila mtu pale ukumbini alikuwa ameridhika na kazi
waliyoifanya majaji.Hakukuwa na aina yoyote ya upendeleo.Baada yakuwatambua warembo wote
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora hatimaye kikafuata kipindi cha maswali.Ni Happy kibaho



.Ni Happy kibaho ...tena ndiye aliyejibu swali vizuri zaidi na kuwafanya watu wote ukumbini kumshangilia kwa
nguvu.Kila mtu alikuwa akiamni kuwa Happy ni lazima angeibuka kuwa mrembo wa Taifa.patrick jasho
lilikuwa likimtiririka mwilini.alijitahidi kwa kila alivyoweza ili asiweze kuonyesha hali yoyote
ya utofauti pale mezani.Baada ya kipindi cha maswali kumalizika ikafuata burudani moja kisha
muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“mabibi na mabwana ule wakati uliokuwa ukisubiriwa na kila mtu hapa ukumbini naona sasa
umewadia.huu ni wakati wa kumtambua mrembo wetu mpya wa Taifa.Napenda nichukue fursa hii
kuwashukuru sana majaji kwa kazingumu waliyoifanya usiku huu kwa kutuchagulia mrembo mpya wa
Taifa.Kabla sijamkaribisha jaji mkuu kuja kutangaza mshindi wa shindano hili napenda kumkaribisha
mrembo anayemaliza muda wake ili aweze kuongea machache na kuwaaga rasmi kabla hajalivua taji la
Miss Tanzania.”
Helen Daudi mrembo anayemaliza muda wake alipanda jukwaani huku akishangiliwa vilivyo.Alipewa
kipaza sauti na kusogea mbele.
“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,waheshimiwa majaji,waandaaji na wadhamini wote wamashindano
haya habari za usiku.Napenda kwanza kabisa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha mimi kutimiza
moja ya ndoto zangu nayo ni kuwamrembo wa Tanzania.Nawashukuru vile vile wazazi wangu na ndugu
zangu kwa kunipa moyo toka katika hatua za awali za kinyang’anyiro hiki hadi nilipobahatika
kuchukua taji.Mabibi na mabwana kulivaa taji la Miss Tanzania ni mzigo mkubwa.Nimeshuhudia mimi
mwenyewe uzito wa taji hili kubwa la urembo hapa nchini.Yapo mengi ambayo unapaswa kulifanyia
taifa hili ukiwa kama mrembo wa Taifa.Kuna mazuri na magumu yake.Zipo changamoto nyingi ambazo
yakubidi upambane kufa na kupona ili uweze kushinda.Napenda kuishukuru kamati nzima ya Miss
Tanzaina kwa ushirikiano mkubwawalionipa katika kipindi chote nilichokuwa nimevaa taji
hili.Sintaweza kumtaja mmoja mmoja lakini napenda niwashukuru wote kwa ujumla.Napenda niwashukuru
vile vile wadau wote wa sanaa hii ya urembo hapa nchini kwa sapoti yao kubwa
waliyonipa.Wamenisaidia sana kuifahamu sanaa hii ya urembo vizuri.Nawashukuru pia wananchi wote wa
Tanzania kwa kunikubali Nawapenda wote na ninaahidi kushirikiana na mrembo atakayevaa taji hili
usiku huu katika yale yote mazuri niliyokuwa nimeyafanya kwani kulivua taji hili si mwisho wa
kuendeleza yale yote niliyokwisha yafanya wakati niko na taji.Mwishokama binadamu kuna wakati
naweza kuwa nimemkosea huyu na yule kwa namna moja au nyingine.Napenda kuchukua nafasihi kwa
dhati kabisa kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea.Tusameheane na kuanzia usiku huu tuanze
maisha mapya.Ahsanteni sana.”
Alimaliza kutoa machache mrembohuyu akarudi katika kiti chake cha heshima huku akishangiliwa na
watu.’
“naam mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mrembo anayemaliza muda wake.Na sasa ule wakati tuliokuwa
tukiusubiri kwa hamu kubwa ndio umewadia.Ni hivi punde tutaenda kumfahamu mrembo wetu mpya.Naomba
sasa nimwite Mr Jackob Evarist ili aweze kututajia washindi wetu.”
Mr jacob akapanda jukwaani.
“Mabibi na mabwana kama alivyotangulia kusema Mrs Coletha brown kuwa mchuano wa leo ulikuwa mgumu
sana.Tunamshukuru Mungu kuwa tumeweza kumpata mrembo wa taifa licha ya kuwa na wakati mgumu hasa
kutokana na kila mrembo ...

...alivyokuwa amejiandaa.Mabibi namabwana nitaanza kuitangaza nafasi ya tatu
hadi moja.”
Alitulia kidogo kisha akaendelea.
“Nafasi ya tatu imekwenda kwa mrembo nambari 16 winifrida mwasajuki”
alitulia kwanza na kumpisha mrembo huyu apite mbele huku akishangiliwa.
“nafasi ya pili imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 20 Neema Japheti”
Kelele za shangwe zikasikika.Neema binti mwenye ngozi nyeusi yenye kung’aa akapita jukwaani akiwa
ndani ya tabasamu kubwa.
“Na sasa mabibi na mabwana ni nafasi yakwanza.Nafasi ya kwanza imekwenda kwa mrembo mwenyenambari
6 Happy .”
Tangu ukumbi wa Diamond jubileeujengwe hakujwahi tokea shangwe kubwa kama hii ya usiku huu ya
kuushangilia ushindi wa Happy.Mrembo huyu alifanikiwa kuzikonga nyoyo za watu vilivyo.
Patrick alishindwa kujizuia akainuka na kushangilia kwa nguvu sana.
Jukwaani Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakuamini kama ni yeyendiye aliyetangazwa mshindi wa
shindano hili hasa kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo miongoni mwa washiriki.Watu
waliKumbatiana na kupeana mikono ya hongera kuashiria kukubaliana moja kwa moja na maamuzi ya
majaji ya kumchagua Happy kuwa mrembo wa Taifa.Kila mmoja aliamini kuwa happy alistahili kulitwaa
taji lile.
Baada ya kama dakika kumi hivi za hoi hoi na nderemo muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
“mabibi na mabwana nafikiri hoi hoi hoi na nderemo hizi zote ni kuonyesha jinsi gani wote kwa
pamoja tunavyokubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji.Happy kibaho ndiye miss Tanzania wetu
mpya.sasa kinachofuata ni mrembo anayemaliza muda wake kulivua taji na kumvisha mrembo mpya.”
Zoezi hili likafanyika huku likishangiliwa kwa nguvu sana.na baada ya zoezi hili kukamilika...

TO BE CONTINUED

1 comments:

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet