Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imempa ushindi msanii wa filamu za
maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, katika kesi ya kujadili upya umri
wake. Akitangaza ushindi huo jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Twalib Fauz,
ameupa ushindi upande wa utetezi uliopeleka ombi la kuujadili upya umri wa
msanii huyo na kuutupilia mbali umri wa miaka 18 alioandikisha kituo cha polisi
baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba.
SOURCE;BONGO FLAVA MUSIC
No comments:
Post a Comment
Thank you for visiting our website