Julie Minter ameshindwa kabisa kuisamehe nafsi yake, baada ya tukio la mwaka 1998 la kuvuta sigara chumbani, na kuisahau na kusababisha moto kwenye chumba cha mtoto wake Terri Calvesbert ambae alikua na miezi 22 wakati huo, na kumsababishia maumivu na majeraha makubwa.
Julie
Minter, alilazimika kuondoa na kukaa mbali na mtoto wake kwa sababu hawezi
kujisamehe kwa kitendo alichofanya. Anadai hakuwahi kuvuta sigara chumbani, ila
kwa mara ya kwanza amefanya hivyo, na tukio hilo la kuumiza limetokea. Julie
aliachana na baba wa mtoto wake huyo miezi miwili kabla ya moto huo, ila
waliamua kuishi pamoja kama marafiki tu.
Mtoto
Terri kabla ya kuungua na moto. Julie ameeleza kwamba, usiku huo Terry alikua
anasumbua kulala, akambembeleza bila mafanikio, akaamua kuwasha sigara na kuvuta. Aliamua kutoka chumbani kwenda jikoni,
akiacha sigara hiyo chumbani. Akiamini kuwa mtoto atalia, ila atanyamaza na
kulala muda si mrefu. Ila alishangaa kusikia mtoto akizidi kulia kwa nguvu na
alipoingia ndani alikuta moto mkubwa,asijue cha kufanya. ndipo alipoita zima
moto, hata hivyo walipofika walikuta Terri ameshaungua sana. Waokoaji hao
wamekiri hawajawahi kuona mtu aliyeungua sana kama huyo na bado akawa hai.
Terri anavyoonekana sasa, hata hivyo amesema hamalaumu mama yake kwa tukio
lililotokea, ila anasikitika kwamba hajapata nafasi ya kumjua mama yake vizuri, alipata nafasi ya kumuona mara moja miaka minne iliyopita baada ya Julie
kuitwa kwenye kikao, ila baada ya hapo hajawahi kumuona tena. yeye anaamini
hakuna anaestahili lawama juu ya hili. Na alimtumia mama yake ujumbe kumwambia
kuwa, hastahili kujilaumu juu ya hili, kwani yeye ni mama yake, na atabaki uwa mama yake siku zote
Terri anaishi na baba yake Paul na mama yake wa kambo Nikki baada ya mama yake kuhama
na kuamua kukaa mbali na watu wote, ikiwemo Terri hata wazazi wake. Mama huyo
ameamua kuishi maisha kana kwamba hajawahi kua na mtoto, ili aweze kusahau
machungu ya tukio hili. Terri kwa sasa ana miaka 15.
Picha na habari kutoka The Sun
ooh no huyu mama pamoja na kuwa hakukusudia kumuuunguza mwanaye, alistahili kumlea ili kumpa mapenzi anayostahili mtoto kupata toka kwa mamaye, maskini Terry I feel so sorry for her
ReplyDelete