TID
Jana kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo
Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa
kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.
Leo kupitia chanzo chetu, meneja wa Ali Kiba
amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo zilizo zagaa
mtaani.
Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa
kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua Ali Kiba.
"Baada sasa ya taarifa hizo kuifikia familia,
iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna
watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale anapoishi
Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kupeleleza eneo
lile.
Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na
kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya
kuwakamata.
Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli
wao wametumwa kuja kufanya jambo hilo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa
Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja
kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndio
anahusika.
Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi
likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati
ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."
Ameongeza kuwa
TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa
kumuua Ali Kiba.
Ally kiba
habari kamili bofya hapa:
No comments:
Post a Comment
Thank you for visiting our website