Saturday 21 January 2012

Long distance Love Is Killing Me jamani....Naombeni ushauri wenu


Mimi ni msichana, nina umri wa miaka 26, nina boyfriend, na tumeshatambulishana kwa wazazi. Mimi niko nje kimasomo, boyfriend yuko Tanzania. Ila kila mwaka summer hua naenda nyumbani kusalimia. Tatizo langu ni hili, nikiwepo nyumbani Tanzania, mwanaume anakua ananijali, ananiheshimu. Yaani nakua na furaha na amani. Ila nikisharudi shule tu, anaanza vituko, mara yuko na wanawake wengine. Wanawake zake wananitafuta na kunitukana, tunakua kila siku ni ugomvi na hamna amani. Na nikifikia uamuzi wa kumuacha, ananiomba msamaha, anasema anafanya yote hayo kwa sababu niko mbali. Na anasema hawezi kupeleka msichana mwingine kwao, kwa sababu wananijua tayari, na wananipenda sana. Na anasema yeye anaamini future yake iko na mimi tu. Mtu wa hivi nimueleweje jamani?ananipenda kweli? 

9 comments:

  1. duh! huyo hana mapenzi ya kweli wala nini, hainiingiii akilini kwamba kuwa kwako mbali ndo afanye hivyo kama ana mapenzi ya kweli kwako asingependa kuona unaumia,na wala asingependa kuwepo na malumbano ktk mahusiano yenu, na hao wanawake wanapata wapi contact zako? mie naona hana adabu wala mapenzi ya kweli any ways wewe wamjua vizuri zaidi yangu but 4me huyo jamaa sio mkweli na atakuja kukuumiza, akili mkichwa mama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. naungana na wewe mdau s.p.j

      Delete
  2. mwanaume kama anakupenda atakusubiri haya mama endelea kusubiri na ukimwi ndo utajua anakupenda au laah wanawake ebu tuamke jamani

    ReplyDelete
  3. mwanaume yyte anaekupenda kwa dhati hatapenda kukuumiza kbsa hzo no hao wanawake wanazitoa wapi,bt follow ua heart we unaonaje

    ReplyDelete
  4. Mpenzi we achana naye kisa cha kujinyima starehe sababu yake na ye hatulii?Bora ukae single mpaka ukirudi ukimkuta bado katulia haya muendelee lakini kama bado ana wanawake tulia Mwenyezi Mungu atakusaidia utapata mwengine.ANGALIZO MKUMBUKE KUPIMA KILA WAKATI UNAPORUDI KUMTEMBELEA MANAKE ELIMU YAKO ITASHIA KABURINI

    ReplyDelete
  5. duh jaman nnachojua n kwamba true lv waits i thnk huyo mkaka hakupend kivile bali anafungwa na kile kitendo cha kwao wanakujua either anaogopa wazaz wake,lakin kama future yake iko kwako kwann hajitunz,huyo atakuumiza hata ktk ndoa asisingizie long distance

    ReplyDelete
  6. Tatizo lako ulikimbilia umarufu wa huyo mwanamziki wako,haya yote yasing kupata shost! ila pole yako c unataka umarufu kupitia yeye...

    ReplyDelete
  7. kwa upande wangu naona huyo kaka hana mapenzi ya kweli,maana long distance relationship ni kipimo cha kujua kama kweli mtu anakupenda,kukujali na kukuheshimu au lah!! so yeye na hizo sababu zake hazileti mantiki hapa.Chamsingi mamii ni kukaa na kufikiria nini haswa unataka,km kweli mnapendana basi kaa nae na muongelee hili tatizo na ukiona hamna mabadiliko basi me kwa ushauri wangu ungeachana nae mapema na ukafanya ustarabu wako maana atakuja kukuumiza hata huko mbeleni kwa tabia hiyo.

    ReplyDelete
  8. mhhh mi naoana huyo hana mapenzi ya dhati, kwani hata kama uko mbali kama anakupenda na kukuheshimu asingethubutu kukuonyesha kuwa anawanawake wengine na pia asingeruhusu wanawake zake kukutukana ama kuwasiliana na wewe kwa njia yoyote ile, Tafakari, chukua hatua"

    ReplyDelete

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet