Watoto wakiwa sehemu za kuchezea, hii ni moja ya sehemu unaweza kwenda na mwanao
Hii ni Tanzania yetu, wala si ulaya. Siku moja moja si mbaya
Ukiwa nje ya nchi, siku za sikukuu au weekend, utaona wazazi, wakiwa na watoto wao, wakitembea sehemu mbalimbali, madukani, sehemu za michezo..ili mradi familia ipo pamoja.
Ila kwa Tanzania yetu, mara chache utakuta wazazi wametoka na watoto wao, baba atatoka peke yake, au zaidi atatoka na mkewe.
Hebu wazazi tujitahidi weekend moja, baba na mama, tuende sehemu, na watoto wetu. Vitu kama hivi hujenga uhusiano mzuri ndani ya familia.
Angalau 4hours mkae na watoto,katika mazingira ya tofauti na nyumbani then usiku wazazi muende mnakotaka, kama bar, mziki etc..siku hizi Bongo yetu imeendelea banaa..sehemu nyingi tulivu za kukaa kifamilia.Watoto nao wanastahili kutoka, na kufurahi mazingira tofauti na nyumbani.
jamani nimewapenda hao babie Mungu awakuze wamependeza wenyewe had raha....
ReplyDeletets very kutoka na familia ako ni raha sana,briner na mwenzake wamependeza sana
ReplyDeleteKwa kweli tunamshukuru mungu, Tanzania imekua half london, tunapata exposure za kutosha hata tukienda huko kwa wenzetu angalau tongotongo zimetutoka
ReplyDelete