Sunday 6 May 2012

MISS TANZANIA.....FATILIA HADITH HII YENYE UHONDO WAKE

MISS TANZANIA-SEHEMU YA KWANZA

“Patrick amka basi darling inakaribia saa nne sasa”Alisema Veronika kwa sauti laini ya

kubembeleza.

‘Mmmmhhh”Aliguna Patrick,akajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.

“Amka basi bwana uende ukaoge”Alizidi kubembeleza Veronika

Kwa uchovu mwingi Patrick akaamka na kunyoosha mikono yake juu huku akijipinda

“Loh !I’m veeery tired”Akasema kwa uchovu.

“lakini ukishaoga uchovu wote utaisha my darling “Akadakia Vero.

Kwa uvivu Patrick akajiinua kitandani na kuelekea bafuni.Dakika chache baadae alitoka akiwa

amechangamka.

‘Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa najisikia saafi kabisa.Nadhani itabidi kwa sasa nipunguze

muda wa kufanya kazi .Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku kiasi kwamba nakosa

hata muda wa kupumzika.naogopa tukija kuonana nisije kuwa nashindwa kutimiza majukumu yangu kama

mume kwa sababu ya uchovu”

Vero akatabasamu halafu akatoa kicheko cha chini chini na kusema

“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kujaribu kupata muda wa kutosha wa kupumzika.”

“Nitajitahidi baby”

Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrickna kumpeleka sebuleni kupata

stafstahi.

“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .Si unajua

kesho Andrew na vicktoria wameahidi kututembelea”Alisema Veronika wakati wakiendelea kupata chai.

“Mhh Vero we nenda tu mwenyewe mi niache nipumzike bwana”Patrick akajibu

“jamani dear usifanye hivyo naomba bwana unisindikize ,mi naona uvivu kwenda peke yangu”

‘haya mama ,tumalize twende ili tuwahi kurudi”

“Nashukuru dear”

Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.

******************************************************************

Veronika Rugi alikuwa ni binti mrembo mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaaliwa

kichwa kizuri chenye nywele laini,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa

na macho mapana yenye kurembua muda wote.Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu hutatamani

abanduke.Mtoto huyu alijaaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na kifua

chenye kupendeza kilichobeba chucu changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa udenda wakware.Kimwana

huyu mwenye uzuri usiopimika alijaaliwa umbo la utatanishi kuanzia kiunoni kushuka chini.Ni

mabinti wachache sana waliopewaupendeleo wa namna hii na manani..

Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi

kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo wake mkubwa wa uelewa .Ni binti mwenye roho nzuri ya

huruma na upendo asiyependa kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo mkubwa familia yake ilionao.Ni

binti mwenye heshima kwa watu wa rika zote ,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote ni mtu

anayejua kupenda.

Veronika ambaye bado anaishi na mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka kadhaa iliyopita

,alikuwa ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ambayo haikubahatika kuwa na mtoto wa
kiume.Dada mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi sasa anafanya kazi ...


...katika shirika la ndege la

British airways ,ameolewa na anaishi nchini Uingereza.Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hii ni

ni binti mrembo sana Sarah ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika kinyan’anyiro cha kumsaka

mrembo wa taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini iitwayo

African meckat bank.Mtoto wa tatuna wa mwisho ni Veronika ambayebado hajaolewa ,ila alikuwa

katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mchumba wake Patrick.Ni hivi

karibuni tu amehitimu shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha dar es salaam.Yeye

ndiye msimamizi mkuu wa miradi yao yote ya familia kwa sasa.

******************************************************************

“basi nikwambie mpenzi nilisahau kukwambia toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana kusikia

kuwa tunataka tukafanye shopping ya harusi yetu nchini Uingrereza,nakwambia alifurahi huyo na

akaahidi kuwa yeye na mumewe watagharamia safari nzima ya kwenda na kurudi na gharama zote za

manunuzi.Amesisitiza kuwa tusitumie hata shilingi yetu.Kwa maana hiyo wiki hii nataka niende tena

kufuatilia yale maombi yetu ya viza pale ubalozini.Nadhani kama Mungu akijaalia basi ndani ya wiki

mbili zijazo tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa.”

Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi na kifua cha Patrick.Muda huo ilipata saa mbili za

usiku na bado walikuwa wakipunga hewa safi baada ya mlo wa jioni.

“Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu sana kama ulivyo

wewe.Tena umeongea kuhusu Loniki nimekumbuka na zile CD alizonitumia wiki iliyopita.Unajua

sijatazama hata moja.Hebu twendendani nikaitazame ile CD mpya ya Jack bauer.”

Alsema Patrick huku akijiinua toka pale walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni .Vero naye

akakusanya vitu vyote vilivyokuwapo hapo chini naye akaingia ndani.

“Vero mbona ile CD ya Jack bauer siioni hapa?au Andrew aliichukua?Aliuliza Patrick baada ya

kuitafuta CD ile bila kuiona.

“Yawezekana Andrew atakuwa aliichukua kwa sababu siku ile aliing’ang;ania sana.Nakumbuka kuna CD

alizichukua hapo nadhani na hiyo nayo ilikuwapo.”Akasema Vero

Patrick akalifunga kabati,akaelekea katika friji akafungua nakujimimia Juice katika glasi .Vero

alikuwa ameketi sofani akitazama Luninga.

“basi nakwambia Patrick ,Miss Tanzania ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa sababu

mabinti ni warembo kupita maelezo.Mhh………..”

Alisema Vero huku amekodoa macho yake katikaLuninga kubwa iliyokuwamo humo sebuleni.

“kwani fainali za miss Tanzania ni lini?”Patrick akauliza

“Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale Diamond Jubilee.Kutapambwa na onyesho kali la machozi

band,vile vile wana Fm academia na wasanii wengine kibao.Nataka kesho nikakate tiketi zetu za V.I

P ili tusikose nafasi siku hiyo”Alisema Vero

Akiwa na juice yake mkononi Patrick akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa Veronika.kabl;a

hajafika sofani alisimama akapiga funda la juice kisha akaelekeza macho yake katika luninga

“Naitwa Neema jastin ni mrembo toka kanda ya kaskazini.Ni miss Arusha.napendelea sana muziki wa
dini,kusoma na ...Itaendelea

...

nitachaguliwa kuwa miss Tanzanianitajikita zaidi katika kuwasaidia watoto yatima kwani naelewa

mateso na machungu wanayaoyapata kwa kutokuwa na wazazi wao.Naombeni kura zenu namba yangu ya

ushiriki ni ishirini.”Alikuwa ni mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi maalum cha

kuwatambulisha washiriki wa kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kilichorushwa moja kwa

moja na televisheni ya Taifa.

“Du! Si mchezo”Aliguna Patrick huku akisogelea zaidi Luninga

“nimekwambia Patrick warembo wa mwaka huu si mchezo .Hebu kaa uangalie jinsi watoto

walivyobomba”Alisema Vero

“Naitwa Happy kibaho.Ni mrembo wa wilaya ya Ilala .Napendelea sana muziki laini,kusoma hadithi

,magazeti,kutazama luninga,na wanyama.nategemea kuwa mwanasheria.Iwapo nitachaguliwakuwa miss

Tanzania nitaelekeza nguvu zangu zote katika kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni pamoja na

kuwatafutia wafadhili,nitaitumia kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu zake zaidi katika

kuwasaidia vijana hawa katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha

ili kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira.Ninaomba kura zenu ili niweze kulitwaa taji

hili la miss Tanzania kwani nina vigezo vyote vya kulitwaa taji hili.Namba yangu ya ushiriki ni

6.”

“Whaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!........................”Patrick Alipiga ukelele

mkubwa

“Nooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!..I cant……………………”alishindwa kuendelea glasi aliyoishika ikamponyoka

na kuvunjika .Taratibu nguvu zikaanza kumwishia akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.

“Patrick ,Patrick what’s wrong!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.........”

Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick pale sofani na kumtingisha.

“Patrick darling what’s wrong withyou?

Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.

“Oooooh!Nooooooooooo!!!!!!!!Wake up Patriick”Alipiga ukelele baada ya kugundua kuwa Patrick hakuwa

na fahamu.Vero akataharuki asijueafanye nini.hakukuwa na mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza

kumsaidia .Alitoka kutaka kwenda kuwaita majirani ,akafika mlangonina kurudi tena ndani mpaka

sofani alipolala Patrick.

“Patrick ,Patrick dear what’s wrongwith you.Whats’s wrong Patrick!!!!!!!!!!!!!!”Vero aliongea

peke yake huku machozi yakimtiririka.Pale pale akapata wazo la kumpeleka Patrick hospitali.Kwa

nguvu zake zote akamuinua Patrick na kumpakia garini,akakimbia kufungua geti kisha akaingia

garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasina kufunga mlango wowote wa nyumba.

Kwa kasi ya ajabu Vero aliendesha gari hadi hospitali ya karibu maarufu kama Dr Heneriko

hospital.Si mbali sana na makazi yaPatrick.Huku akilia akapaki gari na kuingia ndani ,akawaomba

msaada wauguzi .Haraka haraka wauguzi wakamchukua Patrick na kumuwahisha katika chumba maalum kwa

ajili ya kumpatia huduma ya haraka.

“Hurry up.hurry up.Ooh Patrick what’s wrong with you?”Alilalamika Vero kuwaomba manesi waliombeba

Patrick waharakishe.Muda wote huo machozi hayakumkauka.
Veronika alizuiliwa asiingie katika chumba cha huduma ya kwanza ....
...akaachwa hapo nje na mmoja kati ya

manesi akiendelea kumfariji.

“Jipe moyo dada yangu Patrick atapona tu.Mtumaini Mungu.”Nesi yule alimbembeleza Vero kwa upole.

Dakika kama 20 hivi baadae dokta Heneriko alimwita Vero ofisini kwake na kumuomba awe mvumilivu

wakati wakiendelea kuishughulikiahali ya Patrick.Dokta alitaka kufahamu nini hasa kilichopelekea

Patrick kupoteza fahamu.

“Unajua dokta ,Patrick ni mpenzi wangu na tuko katika maandalizi ya harusi yetu.Mimi siishi naye

kwa sasa ila huja kwake kila mwisho wa wiki .Leo hii toka asubuhi alikuwa akilalamika kuwa alihisi

uchovu mwingi .Tulitoka kidogo kisha tukarudi na akaendelea kupumzika.Usiku tukiwa sebuleni

tukiangalia Tv nikaona mwenzangu akipiga ukelele akaishiwa nguvu na kuangukia sofani akapoteza

fahamu.kwa kweli sina hakika mpaka sasa ni kitu gani hasa kilichopelekea hali ile kutokea.Naomba

Dokta ufanye kila linalowezekana iliili Patrick apone.Niko tayari kutoa kiasi chochote cha pesa

ili mradi tu apone.”

Vero alishindwa kujizuia akaanguakilio.

“Nyamaza Vero,Hali ya Patrick inaendelea vizuri. nina hakika muda si mrefu atazinduka.Kwa hiyo

yawezekana kuwa kuna habari yoyote aliyoitazama ambayo haikumfurahisha wakati mkiangalia hadi

ikampelekea yeye kupata mstuko ?

“Sidhani dokta kwa sababu wakatitunaangalia Tv hakukuwa na taarifa yoyote ya kutisha au kustusha

inayoweza kupelekea mtu kupata mstuko hadi kupoteza fahamu.Tulikuwa tukiangalia washiriki wa miss

Tanzania wakijinadi.Ni hilo tu”Veroakajibu

Dokta Heneriko akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema

“Kwa kumbukumbu zako toka umekuwa naye kuna siku yoyote tukio kama hili limewahi kumtokeazaidi ya

leo?

“Hapana dokta tangu mimi nimekuwa naye halijawahi tokea tukio kama hili Patrick kupoteza fahamu.”

“Ok Vero hivi sasa waweza tu kwenda kupumzika na kutuacha sisi tuendelee kumuhudumia mgonjwa

wako.Iwapo kutakuwa na mabailiko yoyote basi tutakupigia simu kukutaarifu.Na kama itahijika

kuhamishwa kupelekwa katika hospitali kubwa zaidi tutakutaarifupia.akini kwa sasa hali yake

inaendelea vizuri,mapigo ya moyo wake yako sawa na kila kitu kinaonekana kufanya kazi vizuri.Huu

ulikuwa ni mstuko wa kawaida tu ambao unaweza kumtokea mtu yeyote na hasa akiwa na msongo wa

mawazo.”Akasema Doctor Henry.

“No Dokta ,siwezi kwenda nyumbani bila kujua hali ya mpenziwangu iko vipi.Nitalala hapa hapa

.Nataka niwe wa kwanza kuniona pindi atakapofumbua macho.Samahani dokta naweza kuitumia simu yako

kuongea na mama yangu na kumtaarifu juu ya ugonjwa wa Patrick”

Dokta Heneriko hakuwa na kipingamizi akamruhusu Vero aitumie simu yake.

Vero akampigia simu mama yake na kumtarifu juu ya tukio lile,halafu akawapigia simu ndugu zake

wote bila kumsahau Andrew rafiki mkubwa wa Patrick pamoja na Aloicy kaka yake Patrick.Wazazi wa

Patrick walikuwa safarini nje ya nchi.

******************************************************************

Ilichukua kama nusu saa hivi toka Andrew apate taarifa ya ugonjwa wa patrick,kuwasili pale

hospitali.Akiwa na mpenzi wake Vick walishuka garini na kukimbia kuelekea mapokezi.Mara tu baada
ya kuingia hapo mapokezi walilakiwa na sura ...


...Vero aliangua kilio ambacho kiliwachanganya zaidi Andrew na Vick.

“Where is Patrick??”Andrew akauliza huku akijikaza lakini ni wazi alikuwa akitetemeka

“Calm down Vero tuambie Patrick yuko wapi?”Aliuliza tena Andrew.Vick akamkumbatia Vero huku naye

machozi yakimtoka.

Andrew alimfuata nesi aliyekuwa mapokezi na kumuuliza juu ya hali ya Patrick.Hakuridhika na jibu

alilolipata ,kwa kasi akakimbia hadikatika ofisi ya Dokta Heneriko lakini hakumkuta.Taratibu

akatoka humo ofisini jaso likimtiririka na kurudi mapokezi.tayari Aloicy kaka yake Patrick

alikwisha wasili hapo hospitali akiwa ameongozana na mke wakenao wote waliungana na Vick katika

kumbembeleza Vero.

Andrew akawasalimia kisha akamvuta mkono alois wakasogea pembeni kidogo.

“Hebu niambie Andrew kitu gani kinachoendelea hapa na Patrick yuko wapi ?

Aliuliza Alocyhuku naye jasho likimtiririka

“Brother Aloicy hata mimi mpaka muda huu sielewe chochote kwanitoka nimefika hapa muda mfupi

uliopita sijaweza kuongea lolote naVero.Ila kwa maelezo niliyoyapata toka kwa nesi ni kwamba

Patrick yuko katika chumba cha huduma ya kwanza akipatiwa matibabu.Nasikia ni mstuko ndio

uliopelekea akapoteza fahamu”

Mara dokta Heneriko akatokea.Nesialiyekuwapo mapokezi akamtambulisha kwa akina Andrew.

“Dokta hawa ni ndugu zake na Patrick wamefika saa hivi na walikuwa wakitaka kupata taarifa juu ya

maendeleo ya mgonjwa wao’

Dr henry akawasalimu wote halafu akawaomba Alois na Andrew wamfuate ofisini kwake..

“Vijana wangu kwanza poleni sanakwa matatizo ‘

“Ahsante sana dokta tumeshapoa”Walijibu kwa pamoja

“sasa vijana wangu nimewaiteni hapa ili tuongelee zaidi suala la ndugu yenu..Patrick aliletwa hapa

kwangu usiku huu akiwa amepoteza fahamu.Kwa haraka nikisaidiana na madokta wenzangu tumejitahidi

kumpatia huduma ya kwanza na mpaka sasa maendelo yake ni mazuri.Tumejitahidi kurekebisha mapigo ya

moyoyaliyokuwa juu sana na kwa sasa yako kawaida.Taratibu anaanza kurejewa na fahamu zakeingawa

bado anahitaji kupumzika zaidi kwani bado fahamu ahizarejea vizuri.Maendeleo yake ni mazuri na

baada ya muda mfupi ujao basi atarejea na fahamu zake zote.”

Alois alishusha pumzi nzito kwa kusikia taarifa ile ya dokta.akatoa leso na kujifuta jasho

lililokuwa likimtirirka kwa kasi muda huo.

“Thanks God”Alisema Alois huku ameinua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu

“kwa hivi sasa bado ataendelea kuwapo katika uangalizi maalum mpaka hapo hali yake itakapokuwa

nzuri kabisa.Tatizo lililompata ni mstuko wa moyo.Ni tatizo la kawaida kutokea.Ila hali yake

itakapokuwa nzuri tutamshauri aonane na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ili aweze kumfanyia

uchunguzi zaidi katika moyo wake ”

Baada ya kupata maelezo ya kutosha toka kwa dokta,Aloicy na andrew waliridhika kabisa na dokta

akawa shauri waende kupumzika mpaka kesho .aloicy alikubaliana na wazo hilo lakini akashauri

andrew awarudishe Vero na Vick nyumbani wakapumzike.Yeye atabaki pale kuangalia hali ya Patrick

inavyokwenda.

Wakati wakiendelea kujadili mama yake Vero akatokea.Akawasalimu wote aliowakuta hapo kisha kwa
wasiwasi akataka kujua juu ya hali ya Patrick.alipewa maelezo na mafupi ya ...

...naye na kupewa kwa muhtasari juu ya hali ya Patrick na

maendeleo yake na akahakikishiwa uangalizi wa hali ya juu.

“Ok jamani sasa utaratibu gani unaoendelea hapa?

Aliuliza Bi stella Rugi mama yake naVero.

“Tumepanga kuwa Andrew awarudishe nyumbani Vero na vickwakapumzike ,mimi nitaendelea kubaki hapa

hapa na kufuatilia hali ya mgonjwa”Alisema aloicy

“Vizuri ,basi msipate shida ,Vero naVick nitaondoka nao mimi,halafu Andrew nenda kule kwa Patrick

ukahakikishe usalama .Aloicy utaendelea kubaki hapa kumwangalia mgonjwa .Nitakuwa nakupigia simu

mara kwa mara ili kujua maendeleao ya mgonjwa sawa baba eenh”Alisema mama yake Vero

“sawa mama tumekuelewa.”Andrew na aloicy waliitika kisha wote wakatawanyika na kumwacha Aloicy

hapo hospitali

Saa saba usiku Patrick akarejewa na fahamu zake kamili.Kitu cha kwanza kuhisi ni harufu kali ya

dawa.akageuza shingo kutazama pande zote akatambua kuwa pale alikuwa hospitali.Taratibu akavuta

kumbukumbu za nyuma na mara akakumbuka kitu kilichopelekea yeye kuwepo pale.

“I saw her.Real I saw her.she’s alive”Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na

mapigo yake ya moyo kwenda kasi.

“I saw her.Real I saw her.she’s alive”Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na

mapigo yake ya moyo kwenda kasi.Muuguzi aliyekuwa akimuangalia aliingia ndani na kumkuta tayari

Patrick amerejewa na fahamu na amekaa kitandani.Haraka akaenda kumwita daktari.Dk heneriko alikuja

kwa kasi na kumpima akagundua kuwa bado mapigo ya moyo wa Patrick yalikuwa juu sana.

‘Lazima kuna kitu kinamsumbua huyu si bure”Aliwaza dokta Heneriko.

“Patrick “Dokta akamwita baada yakumaliza kumfanyia vipimo.

“naam dokta”Aliitika Patrick kwa sauti yenye kukwaruza.

“Pole sana “

“Ahsante sana dokta”

“Patrick kijana wangu usijali utapona tu hali yako inaendelea vizuri .Unahitaji kupumzika sasa

mpaka hapo asubuhi tutakapochukua tena vipimo vingine”

“Sawa dokta.”

“Ok pumzika Patrick na iwapo utahitaji kitu chochote nesi yuko hapo nje na atakuwa akija hapa mara

kwa mara kukuangalia.Tena nimekumbuka kaka yako yuko nje muda sasa sijui kama ungependa

kumwona?”Akasema dokta heneriko.

“Yes dokta naomba uniitie..”

Dokta Heneriko akafungua mlango na kutoka.

Alois muda huo alikuwa amesinzia katika sofa lililoko mapokezi Mara akastuliwa na sauti ya Dokta

Heneriko.

“Alois,Patrick amekwisha rejewa na fahamu zake kamili kwa hiyo unaweza kwenda kumwona.Ila

tafadhali usijaribu kumuuliza chochote kuhusiana na kilichopelekea yeye kupoteza fahamu.Ongea naye

maongezi mengine ya kawaida.sawa?”

“sawa dokta”Alijibu Patrick huku akifikicha macho yaliyojaa usingizi.Nesi aliyekuwepo mapokezi

akampeleka hadi katika chumba alimokuwa amelazwa Patrick.

“Vipi brother unajisikiaje kwa sasa?Alisema Alois

“Sasa hivi sijambo brother najisikiavizuri.nashukuru kwa kuja kuniona”

“Usijali Patrick kwa sasa endelea kupumzika.bado unahitaji mapumziko ya kutosha.Mimi niko hapo

mapokezi tutaonana asubuhi”

“Ok brother”

.

..kiusingizi kikaanza kumchukua na taratibu akajikuta akianza

kulala.Hazikupita hata dakika kumi toka aanze kusinzia simu yake ikaanza kuita na kumstua toka

usingizini.Alipoiangalia simu yake ilikuwa imeandika jina Alois.Aliogopa kuipokea simu ile akabaki

akiiangalia ikiiendelea kuita.Mikono ilikuwa ikimtetemeka.Alihofia pengine simu ile inaweza kuwa

imebeba ujumbe mbaya kuhusu Patrick.Simu iliita ikakatika ,ikaanzakuita tena.Akaamua kuipokea.

“Haloo”Aliita Vero

“Haloo shemeji vipi?Ilkuwa ni sautiya upande wa pili wa simu ambayoVero aliitambua moja kwa moja

kuwa ilikuwa ya Alois.

“safi shemeji vipi kwema huko?Alisema vero huku mapigo yake ya moyo yakienda kwa kasi isiyo ya

kawaida.

“Huku kwema tu shemeji.Nataka nikufahamishe tu kuwa Patrick tayari amekwisha rejewa na fahamu zake

na nimetoka kuongea naye muda si mrefu.Kwa hivi sasa anaendelea kupumzika.kwa hiyo shemeji yangu

unaweza ukalala kwa amani sasa.”

Vero akashusha pumzi ndefu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamuaga Aloicy na kukata

simu.Alipokata simu akaanza tena kulia kwa kwikwi..Vick ambaye alikuwa katia usingizi mzito

akaamka baada ya kustushwa na kilio cha Vero.

“Vero nini tena?

“Patrick anaendelea vizuri.Alois amenipigia simu sasa hivi na kunifahamisha.”

“sasa kama hajambo unalia nini?

“Huwezi jua Vick ni jinsi gani nisivyopenda kumuona Patrick akiumwa kwa jinsi

ninavyompenda..Ninalia kwa mateso ninayoyapata juu yake.”

Vick alimbembeleza vero hadi akanyamaza kisha akajilaza kitandani na kuanza kutafakari.juu ya

tukio zima..Alikumbuka walikuwa sebuleni wakiangalia luninga ambapo warembo wanaotarajia kuwania

taji al miss Tanzania walikuwa wakijinadi .alivuta picha na kumuona Patrick akiwa katka friji

akijimiminia maji katika glasi ambapo muda huo Miss arusha Neema aliikuwa akijinadi.Alikumbuka

kumuona Patrick alivyovutiwa ghafla na kipindi hicho cha warembo.Toka Neema hakumbuki ni mrembo

gani aliyefuatia kujinadi ila anachokumbuka ni kwamba Patrick alipiga ukelele mkubwa wa kama

anashangaa kitu halafu akaanguka.

“Ni dhahiri ni mstuko ndio uliomfanya Patrick aanguke na kupoteza fahamu .Lakini je ni kitu ganui

hasa ambacho kilimstua Patrick kiasi cha kupoteza fahamu?Je mstuko huu una uhusiano wowote na

kipindi kile tulichokuwa tukikitazama?Lakini hapana Patricknimekuwa naye kwa muda mrefu sasa na

tabia yake ninaifahamu vizuri.Kuhusu wanawake siwezi kumsemea vibaya hana tabia hiyo ya kuwa na

wanawake wengine nje ya mahusiano yetu.Nina uhakika na hilo.Sasa ni kitu gani alistuka ?any way

siwezi kupata jibu kwa sasa mpaka hapo atakaponiambia yeye mwenyewe kwani nina hakika hawezi

kunificha kitu chochote.”

Alikuwa akiwaza Vero na taratibu usingizi ukamchukua akalala.

*****************************************************************

Saa kumi na mbili asubuhi iliwakuta Vero ,Vick na mama yake vero hospitali.Hali ya Patrick ilikuwa

ikiendelea vizuri .alfajiri hiyo tayari alikwisha hamishwa toka katika chumba cha uangalizi maalum

na kuwekwa katika chumba cha mapumziko ya kawaida.

Wakiongozwa na alois ambaye alilala hapo hospitali walielekea moja kwa moja chumbani na kumkuta


Patrick tayari amekwishaamka.Bila kupoteza muda Vero akamkumbatia na kumpiga mabusu mfululizo.

“Pole sana my dear.Unajisikiaje kwa sasa?

“Najisikia vizuri sana”

... alijibu Patrick huku akijinyoosha nyoosha pale kitandani.baada ya kusalimiana kilifuata kipindi

cha vicheko na utani wa hapa na pale kisha Vick na mama yake Verowkaomba waondoke kwa ajili ya

kwenda kujiandaa na mishughuliko ya siku.

Vero alimwinua Patrick na kumpeleka bafuni ambako alimwogesha na kumrudisha tena chumbani

,akamwandalia kifungua kinywa.Patrick alijisikia faraja kubwa kwa jisni binti huyu alivyokuwa

kimuhudumia.

****************************************************************

“Andrew kwa kipindi kirefu sasa umekuwa ni msiri wangu mkubwa.Mambo yangu mengi ambayo sihitaji

mtu mwingine kufahamu wewe wayajua.Urafiki wetu ni zaidi ya undugu.Naomba sana kile

nitakachokuambia hapa usimwambie mtu yeyote yule.Itabaki kuwa siri yako mpaka pale muda muafaka

utakapofika.”

Patrick aliongea taratibu huku akijiweka vizuri sofani.Ni siku ya kwanza tangu ameruhusiwa kutoka

hospitali kwa sababu ya mstuko uliopelekea apoteze fahamu.Andrew rafiki mkubwa waPatrick alikuwa

kimya akiwa na shauku kubwa ya kutaka kulisikia lile ambalo rafiki yake alikuwa tayari kumwambia.

“I saw Happy”alisema Patrick kishaakatulia na kuyaacha maneno yale yamwingie Andrew.

“what” aliuliza Andrew kwa mshangao

“I saw Happy”

Patrick alirudia tena kisha akainamisha kichwa chini na kuzama katika mawazo mazito.andrew

aliinuka na kuanza kuzunguka zunguka mle chumbani huku akionekana dhahiri alikuwa meshtushwa mno

na kauli ile ya Patrick.

“Umemuona wapi?”andrew akauliza huku amejishika kichwa.

‘Nimemuona kwenye tv .Kulikuwa na kipindi cha kuwanandi warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro cha

kumsaka mrembo wa Taifa .Happy ni miss Ilala.”
“are you ...



...sure” Andrew akahoji

“Yes I'm sure na ndio kitu kilichonifanya nikapata mstuko na kupoteza fahamu”

Andrew alivuta pumzi ndefu,akainuka akaanza kuzunguka zunguka humo ndani kisha akakaa.Vijana hawa

wote kwa sasa walikuwa katika wakati mgumu sana.Ni Andrew pekee aliyefahamu kilichokuwa

kikiendelea kati ya Patrick na Happy na ndio maana alichanganyikiwa asijue afanye nini.Alimuonea

huruma sana Patrick kwa wakati huu mgumu alionao.

“Vero aligundua chochote “Andrew akauliza tena

“sidhani kama aligundua kitu chochote.sidhani kama alihisi chochote kwa wakati ule”

“Ok kwa hiyo tufanye nini sasa” Andrew alihoji.

Patrick akainuka na kwenda katikafriji akjimiminia maji baridi kwenyeglasi akapiga funda kubwa

kisha akavuta pumzi ndefu na kusema.

“Nataka kuonana na Happy”

Kimya kikatanda hapo sebuleni

“Nataka kabla ya kuonana naye kwanza tumfanyie uchunguzi anaishi wapi,na nani anafanya kazi

gani,ana mchumba hana,na chochote kile tunachoweza kukifahamu kuhusu yeye.Uchunguzi huu nataka uwe

wa siri na yeye Happy asiweze kufahamu kuwa anachunguzwa.Ikiwezekana tunaweza hata kuajiri mtu wa

kuifanya kazi hii niko tayari kumlipa kiasi chochote cha pesa anachohitaji.Nakukabidhi kazi hii

Andrew nina imani itafanyika ipasavyo.Tuko pamoja?

“Nimekuelewa Patrick lakini suala hili haliwezi kuathiri maandalizi ya harusi yako ambayo tayari

yamekwishaanza?”

“Hahahah usihofu kuhusu hilo my friend.I know what I’m doing ,ok?”

“Una maana gani Patrick unaposema unajua unachokifanya?Ninafahamu kuwa ndoto zako za siku nyingi

ni kuwa na Happy katika maisha yako na kwa sasa umekwisha kuwa na uhakika kuwa yupo na kwa wakati

wowote unaweza kumuona .Nina wasiwasi sana na huu ujio wa Happy katikati ya maandalizi ya Harusi

yako unaweza kutibua kila kitu.

“Kwa ajili ya Happy niko tayari kwalolote linaloweza kutokea.I must fight for her.all these years

I’ve been hurting myself thinking about her na mpaka sasa nimeshindwa kabisa kuifuta kumbukumbu

ya Happy moyoni mwangu.Siwezi kuendelea kuutesa moyo wangu Andrew.I have to face her.” Akasema

Patrick

“Patrick nafikiri unahitaji kufikiri zaidi kuhusu suala hili, si suala jepesi kama

unavyolifikiri.Ni suala ambalo linagusa hisia za watu wengi.Hi…..”

Andrew hakuendela Patrick akadakia.

“Andrew no body’s gonna change my mind.That’s my decision and itsfinal.Nilivyoamua

nimeamua.Nitapambana kadiri ninavyoweza ili kumpata Happy.I love her and I know that she loves me

too.”

“Patrick miaka mingi imepita tangumpotezane na Happy na kwa sasa bado kama mwezi mmoja na nusu

hivi ufunge ndoa na Vero ,ndoa ambayo sehemu kubwa ya maandalizi yake yamekamilika.Huoni kuwa

utakuwa unamyima haki zake Verokama ukihamishia mawazao yako yote kwa Happy.?Nina imani Vero

anakupenda kwa dhati ya moyo wake na nina imani vile vile hata wewe unampenda Vero sasa kwa nini

utake kumtesa hivi mtoto wa watu?

“Andrew unayasema haya yote kwa sababu huwezi kuingia katikaviatu vyangu na kuona nini kilichomo

ndani.Nina imani kubwa hata wewe ungekuwa mahala pangu kwa sasa basi ungeweza kufanya kama mimi

ninavyofanya.Please Andrew naomba msaada wako katika hili.Ni lazima nionane na happy hivi

karibuni.”

“Nimekuelewa Patrick lakini bado moyo wangu una wasiwasi sana juu ya kinachoweza kutokea.hapo

...
ITAENDELEA ..

No comments:

Post a Comment

Thank you for visiting our website

Wazoefu Computer Technology

Search This Blog

Please Share This

Thanks for Like and Tweet